
RAMIRES amejiunga rasmi na klabu ya Jiangsu Suning
ya China kwa mkataba unaokadiriwa kuwa na thamani ya paundi milioni 25.
Jiangsu walimaliza katika nafasi ya tisa katika
msimamo wa Ligi Kuu ya China mwaka jana na wanafundishwa na beki wa zamani wa
Chelsea Dan Petrescu.
Ramires aliisaidia Chelsea kunyakuwa taji la moja la
Ligi Kuu, Kombe la FA, Kombe la Ligi, Ligi ya Mabingwa Ulaya na Europa League.
Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa
miaka 28, alisajiliwa Chelsea akitokea Benfica kwa kitita cha paundi milioni 17
mwaka 2010.
Post a Comment