Halloween Costume ideas 2015

TANGAZA NASI.

TANGAZA NASI.

YANGA SASA KELEKA TANGA WALA SIO AFRIKA KUSINI KAMA WALIVYOPANGA.



 
Klabu ya soka ya Yanga imeahirisha safari ya Afrika Kusini sasa kubadiri muelekeo wao na kuelekea Tanga kwa ajili ya mchezo wao wa jumamosi wa Ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Coastal Union.


Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano cha klabu ya soka ya Yanga Jerry Muro amesema hawataenda Afrika Kusini na baadala yake wanaelekea mjini Tanga katika mchezo wao dhidi ya Coausta.

Muro amesema wameamua kwenda Tanga baada ya kunyimwa kibari na Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF cha kusafiria hivyo wanakwenda Tanga kwaajili ya mchezo wao huo wa jumamosi.

Klabu ya Yanga ilitaka kwenda Afrika Kusini kwaajili ya kujiandaa na mchezo wake wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Cercle de Joachim ya Mauritius utakaopigwa Februari 13, nchini Mauritius.

Na hatua hii imekuja baada ya klabu ya soka ya ya Azam kupewa ruhusa na TFF kuelekea nchini Zambia kwaajili ya kucheza michezo ya kirafiki kwaajili ya mashindano yao ya kombe la shirikisho.

Post a Comment

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget