Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Kassim Majaliwa ameshangazwa na Shirikisho la soka nchini kumrudisha tena Kim
Poulsen kuwa kocha mkuu wa timu ya vijana hapa nchini.
TFF kupitia kwa Rais wake Jamali Malinzi mapema
mwaka huu alimtangaza kocha huyo kuwa kocha mkuu timu ya vijana nchini.
Waziri Majaliwa alishangazwa kusikia hivyo kuhoji ni
TFF ilimrudisha kocha huyo ilihari walishamtimua kutokana na kuleta matokeo
mabovu katika timu ya wakubwa ya Taifa Stars.
Na aliyasema hayo wakati alipokutana na vyama vya
michezo mbalimbali hapa nchini siku ya jana kwa ajili ya kujua changamoto mbalimbali
zinazosumbua katika vyama hivyo na zinazosababisha kushindwa kufanya vizuri
kimataifa.
Post a Comment