
Kocha mkuu wa klabu ya Manchester United Louis Van
Gaal amethibitisha kuwa Nahodha wake Wayne Rooney amepata majeraha na na atakuwa
nje dimba kwa wiki tatu hadi nne.
Van Gaal amesema Nahodha wake huyo amepata majeraha
ya goti wakati wa mchezo wao wa ligi kuu soka nchini Eingland dhidi ya Sunderland
wiki iliyopita.
Van Gaaal amesema kikosi chake cha Manchester United
kinasfiri kuelekea Denmark kuifuata Midtjylland kwa ajili ya mechi ya michuano ya
Europa Cup.
Kuumia kwa Rooney kunamfanya akose mchezo huo wa
Europa Cup huku akiwa amefunga mabo 7 katika mechi 9 alizocheza katika klabu
yake.
Post a Comment