Halloween Costume ideas 2015

TANGAZA NASI.

TANGAZA NASI.

SOMA BARUA HII KWENDA KWA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI TFF.


 
Na Godfrey Mbai

Watani wa jadi katika soka la Bongo Yanga na Simba wanakutana jumamosi hii katika mechi inayosubiriwa kwa hamu kote nchini ya mzunguko wa pili wa Ligi kuu Bara.

Tayari joto na presha ya mechi hiyo imeanza kupanda tangu wiki mbili zilizopita huku kila upande ukijinadi kuibuka na ushindi katika mechi hiyo yenye kutawaliwa na vituko vya kila aina ndani na nje ya uwanja.

Kuelekea katika mtanang’e huo Shirikisho la soka nchini(TFF),mwanzoni wa wiki hii liliweka wazi viingilio vya mechi hiyo huku kile cha chini kikiwa ni shilingi elfu saba.

Viingilio vingine ikiwa ni  kama vile ,kiingilio cha juu cha mchezo huo ni shilingi Elfu Thelathini (30,000) kwa VIP A, Elfu Ishirini (20,000) VIP B & C, Elfu Kumi (10,000) kwa vile vya rangi ya machungwa (Orange), na Elfu Saba (7,000) kwa viti vya rangi ya bluu na kijani.

Katika makala hii tutaangalia ni kwa namna gani mechi hii inafanya kiingilio cha elfu saba kukubalika miongoni wa wadau wa soka nchini kuwa kiingilio cha chini kabisa katika mechi hiyo huku mechi nyingine zikiwa na viingilio vya chini vya  kawaida zikiwemo zile zinazohusisha Yanga na Simba dhidi ya timu nyingine tofauti na zinapokutana zenyewe.
Ukongwe wa timu hizo

Hakuna ubishi ata mtoto wa miaka kumi anajua kuwa Yanga na Simba ndio timu kongwe na zilizodumu kwa muda mrefu katika soka la Bongo licha ya changamoto za hapa na pale.Yanga ikizaliwa 1935 huku Simba yenyewe ikisimama 1936  kwa kupita katika majina kadhaa kama vile Sunderland na kadhalika.

Ukongwe wa timu hizi na idadi kubwa ya mashabiki walionao unafanya  kiingilio cha chini cha elfu saba au ata  elfu15 kukubalika kirahisi na mashabiki kujitokeza  kuwatazama wakongwe hao.

Ukubwa wa mechi na nafasi za timu hizo katika msimamo wa ligi

Hii inaweza kuwa sababu nyingine ambayo inapekea Tff kufanya kiingilio cha chini kuwa shilingi elfu saba au zaidi nab ado kukubalika na wapenzi wa timu hizo nchini na kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa.

Licha ya kuwa na wakati mgumu chini ya kocha Kerr Simba wanaingia katika mechi ya jumamosi dhidi ya Yanga wakiwa kileleni mwa msimamo(shukrani kwa mabadiliko ya ratiba),wakiwa na alama 46 baada ya mechi 19 huku Yanga wakiwa nafasi ya pili na alama 42  katika mechi 18.

Hivyo mashabiki watakua na shauku ya kufika Taifa ili kujua kama Yanga watapata alama tatu na kuifukuzia Simba au Mnyama ata pata alama tatu au moja  na kuendelea kusalia kileleni huku wakisubiri Yanga na Azam wacheze viporo vyao?,hapa washabiki hawana namna zaidi ya kukubali elfu saba au zaidi kama kiingilio cha chini ili tu kupata burudani na kujua hali ilivyo kimsimamo kwa timu hizo katika ligi.

Hakuna mechi nyingine yenye kuvuta hisia za wapenda soka nchini

Licha ya Azam kuonekana kuleta upinzani dhidi ya vigogo ,ukweli unabaki wazi kuwa pambano kati ya wakongwe hawa linabeba hisia za wapenda soka kote nchini.

Kuanzia viongozi,wanachama na mashabiki wa pande zote mbili huwa katika vihoro kabla na baada ya mechi hiyo.

Vyombo vya habari ndio usiseme,wiki mmoja kabla ya mechi magazeti,televisheni,radio na mitandao mbalimbali ya kijamii hutawaliwa na taarifa za Yanga na Simba, na ata baada ya mechi kwisha mengi husemwa na kuandikwa juu ya pambano hilo,kwanini usiweke elfu saba au zaidi ya hapo kuwa kiingilio cha chini wakati kuna mechi mbili tu katika msimu mzima wa ligi kuu zenye kuvuta hisia nazo ni Yanga na Simba au Simba na Yanga(nyumbani na Ugenni).

Matokeo ya mechi iliyopita

Septemba mwaka jana katika mechi ya mzunguko wa kwanza Yanga ilipata ushindi wa 2-0 dhidi ya watani zake Simba katika dimba la Taifa.Magoli ya Amis Tambwe na Malimi Busungu yalitosha kupeleka furaha Jangwani na kupeleka huzuni Msimbazi.
Matokeo haya ya mechi ya kwanza yanawapa viburi mashabiki wa Yanga hivyo kwao inakua rahisi kujitokeza uwanjani wakiamnini timu yao itaendeleza ubabe huku wale wa Simba wakipata nguvu na matokeo ya siku za karibuni ya timu yao chini ya kocha Mayanja, hivyo kupata kiburi cha kwenda Taifa wakiwa na imani ya kupata ushindi.Hapa elfu saba au 15 kama kiingilio cha chini kabisa bado watu watajaa wa pande zote mbili kila upande ukiamini kuibuka kidedea.

Kuimairishwa kwa ulinzi

Kati ya mechi za ligi kuu Bara ambazo ulinzi uimarishwa na vyombo husika basi hii ya Simba na Yanga ulinzi huwa wa hali ya juu kwa upande wa watu na mali zao ndani nan je ya uwanja.

Vikosi vya kulinda usalama na kutuliza ghasia umwagika kwa wingi katika dimba la taifa ndani na nje kwa lengo la kuhakikisha kuwa kila kitu kinakwenda sawa.

Watu wa Msalaba Mwekundu huwa tayari kutoa huduma popote pale ndani ya uwanja na nje pindi tatizo linapotokea.

Ata jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Daressalaam lilisikika likigusia juu ya hali ya kuimarishwa kwa ulinzi na usalama kuelekea mechi hiyo.

Hapa kwa mpenzi wa soka ni rahisi kukubali kiingilio cha chini kuwa elfu saba au kumi na tano kwa kuwa tu kuna uhakika wa usalama wa yeye  na mali zake siku ya mchezo,hapa ndipo Tff wanacheza na akili za watanzania na kuamini wataenda tu katika dimba la Taifa kutazama mchezo huo.

Mwandishi wa Makala ni Mtangazaji wa zamani wa kipindi cha Anga za Michezo cha Radio SAUT Fm.Mwandishi mchangiaji katika magazeti mbalimbali kama vile Kiongozi,Habari Leo,Jamhuri,Mwanaspoti,Mbiu ya Jamii na Mdadisi.Pia aliwai kufanya kazi kwa mda mchache katika Radio ya ABM ya Abdallah Majura. Kwa sasa ni mfanyakazi katika kampuni ya Choice Int’l Forwarding Co,Ltd.

Anapatikana katika 0718-529068 au mbaigodfrey@gmail.com

Post a Comment

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget