
Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Real Madrid
Cristiano Ronaldo amethibitisha ubora wake baada ya kuisaidia timu yake kuibuka
na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya walipokuwa
ugeni dhini ya AS Roma.
Ronaldo jana alionekana moto wa kuotea mbali na
kudhihirisha kuwa anaweza kupachika mabao akiwa nyumbani na hata ugenini baada
ya juzi kuulizwa swali na waandishi wa habari kuwa kwanini hafungi mabao akiwa
ugenini kisa kilichopeliekea kuondoka akiwa katika mkutano huo bila kujibu
swali hilo.
Pamoja na Ronaldo kukwamisha bao moja kimianai lakini
nyota mwingine wa klabu hiyo Jesse naye akimalizia kukomelea msumari
wa moto kwenye lango la Roma na kuiwezesha timu yake kutoka na ushindi wa mabao
2-0.

Klabu ya Madridi chini ya kocha wake Zinadine Zidane
ilifanikiwa kupata ushindi huo ugenini na kuifanya iendelea kuwa na rekodi
nzuri katika hatua ya makundi.

Post a Comment