Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo,
Nape Nnauye ametengua uteuzi wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania
Henry Lihaya baada ya kushindwa kutekeleza wajibu wake.
Mhe. Nnauye alitengua uteuzi huo katika ziara yake aliyoifanya leo mapema katika ofisi za BMT kuona miundo mbinu ya ofisi hizo na kujua changamoto walizonazo.
Aliongeza kwa kusema kuwa, miaka saba ambayo Lihaya
amekuwa Katibu Mtendaji wa Baraza imetosha kwani hakuna mabadiliko yoyote
aliyoyafanya katika sekta ya michezo tangu alipoteuliwa mwaka 2009.
Baada ya Mhe. Nnauye kufanya utumbuaji huo wa jipu sasa nafasi ya hiyo ya katibu wa BMT imechukuliwa na Said kaganja kuwa kaimu mtendaji mpya.
Baada ya Mhe. Nnauye kufanya utumbuaji huo wa jipu sasa nafasi ya hiyo ya katibu wa BMT imechukuliwa na Said kaganja kuwa kaimu mtendaji mpya.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa BMT Dionis Malinzi amesema
uteuzi huo ni kwa mujibu wa sheria ya BMT namba 12 ya 1967 kifungu namba 5(1)
baada ya kupata idhini ya Waziri mwenye dhamana.
UZOEFU
WA SAID KIGANJA KATIKA MICHEZO.
kabla ya uteuzi huo Kiganja alikuwa Afisa michezo Mkuu katika ofisi ya Rais,Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) kuanzia mwaka jana mpaka uteuzi wake leo hii ulipofanyika.
kabla ya uteuzi huo Kiganja alikuwa Afisa michezo Mkuu katika ofisi ya Rais,Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) kuanzia mwaka jana mpaka uteuzi wake leo hii ulipofanyika.
Pia kiganja aliwahi kufanya kazi kama Afisa
mwandamizi wa michezo wa Baraza la michezo Tanzania na Afisa michezo Mkuu
katika ofisi ya Waziri mkuu.
Kaganja ana shahada ya kwanza ya Elimu katika
masuala ya michezo na Utamaduni kutoka katika chuo cha Dar es Salaa.
Aidha, Mhe. Nnauye amemuagiza Katibu Mkuu wa wizara
ya habari, utamaduni sanaa na michezo kumpangia Lihaya kazi nyingine ya kufanya
wizarani.
Post a Comment