Timu ya Acacia Stand United fc (CHAMA LA WANA) imejidhatiti vilivyo kuelekea mchezo wake wa kesho wa ligi kuu soka Tanzania Bara dhidi ya Maafande wa jeshi la kujenga taifa JKT Ruvu kutoka Pwani.
Acacia Stand United Fc kesho
inashuka dimbani katika uwanja wake wa nyumbani CCM Kambarage mjini shinyanga
kucheza na JKT Ruvu ikiwa ni muendelezo wa michezo ya ligi kuu soka
Tanzania Bara.
Afisa habari wa “CHAMA LA WANA”ISAAC EDWARD amesema wako vizuri kuwaangamiza maafande hao na kuzoa pointi zote tatu ili kuwapa furaha mashabiki wao ambayo waliikosa katika mchezo wao uliopita walipofungwa nyumbani dhidi ya Simba sc.
Afisa habari wa “CHAMA LA WANA”ISAAC EDWARD amesema wako vizuri kuwaangamiza maafande hao na kuzoa pointi zote tatu ili kuwapa furaha mashabiki wao ambayo waliikosa katika mchezo wao uliopita walipofungwa nyumbani dhidi ya Simba sc.
“kiukweli tumejidhatiti vilivyo
kuelekea mchezo wetu wa kesho dhidi ya JKT Ruvu,tuna kila sababu ya kushinda
mchezo huo licha ya kuwa maafande hao wana kikosi kizuri na benchi la ufundi
lenye watu wazoefu na soka la Tanzania lakini haitakuwa sababu ya kushindwa
kuwapa kichapo”
Edward ameongeza kuwa kikosi chao
kinazidi kuimalika kila kukicha na pia ujio wa wachezaji wao Haruna
Chanongo na Abuu Ubwa kambini umeongeza Morali kambini.
Pia amewaomba mashabiki na wapenzi
wa klabu hiyo pendwa mkoani shinyanga kujitokeza kwa wingi kuishangilia kwani
katika kipindi hiki cha mzunguko wa pili wa ligi,timu inahitaji sana kupata
ushirikiano mkubwa kutoka kwao ili ifanye vizuri katika michezo yake ijayo na
hatimae kushika nafasi za juu pindi ligi itakapo fikia tamati.
tuweze kukaa katika nafasi nzuri
kwenye msimamo wa ligi na hasa katika kipindi hiki cha mzunguko wa pili wa ligi
timu inahitaji sana sapoti ya mashabiki tufanikishe kushinda mechi zilizobaki
na hatimae mwisho wa ligi tukae katika nafasi za juu”
Post a Comment