
Klabu ya soka ya Arsenal inajiandaa kuizidi kete klabu
ya Manchester United katika mbio za kumtwaa mshambuliaji wa klabu ya Napoli Gonzalo
Higuain.
The Gunners' ilishindwa kumsajili mchezaji huyo katika
msimu wa mwanzoni wa ligi kuu 2015-16 na mashabiki wa klabu hiyo waliilaumu klabu
yao kushindwa kumsajili mchezaji huyo mwenye adhi ya dunia.
Hata hivyo kocha Arsene Wenger ameshaanza kumtolea
macho Higuain, ambaye amepachika mabao 29 katika mashindano yote msimu huu.
Arsenal watakumbana na ushindano kutoka kwa United,ambao
wametoa ofa ya £85 million kwa ajili ya kumtwaa mchezaji huyo raia wa nchini Argentine.
Post a Comment