
Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Manchester United Anthony
Martial anaimani kuwa ligi ya nchini Uingereza ni ligi bora duniani kote na
anaimani kuendelea kubaki nchini Uingereza katika maisha yake yote.
Mshambuliaji huyo ambaye ni raia wa nchini Ufaransa
alijiunga na klabu ya Manchester United akitokea Monaco mwanzoni mwa msimu wa ligi hiyo 2015-16
ana ameonyesha kiwango bora zaidi katika viunga vya Old Trafford na amepachika
mabao 12 katika mashindano yote.
Vijana wa Louis van Gaal's hivi sasa wapo katika
hatari ya kuikosa michuano ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya katika msimu ujao
lakini Martial atajitaidi kuisaidia klabu yake kufanya vizuri zaidi.
Amesema ligi ya Uingereza inautofauti mkubwa na ligi zingine kutokana na uimara wake kwa kuwajenga wachezaji wanoshiriki ligi hiyo.
Post a Comment