
Klabu za Manchester United na Liverpool zimeshtakiwa
na Uefa kufuatia fujo za mashabiki wakati wa mechi ya marudiano ya Europa
League iliyochezwa Alhamisi.
Klabu hizo zilitoka sare bao1-1 na mechi hiyo ya
marudiano ya hatua ya 16 bora iliyochezewa uwanja wa Old Trafford.
Mashabiki wa timu zote mbili walionekana
wakikabiliana uwanjani na viti vilirushwa na mienge kuwashwa wakati wa mechi
hiyo.
Katika fujo hizo takribani Watu watano walikamatwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi.
Klabu zote mbili zimeshtakiwa na makosa ya mashabiki
kuzua fujo pamoja na vitu kurushwa uwanjani.
Manchester United pia wanatuhumiwa kufunga ngazi nao
Liverpool wanatuhumiwa kuchelewesha mechi, mashabiki kurusha matusi na kuwasha
mienge.
Liverpool walisonga kwa jumla ya mabao 3-1 kutokana
na ushindi wao wa 2-0 mechi ya mkondo wa kwanza.
Kesi hiyo itasikizwa na bodi ya nidhamu ya Uefa
mnamo 19 Mei, siku ambayo fainali ya Europa League itakuwa ikichezwa mjini
Basel.
Post a Comment