
KLABU ya Stoke City inadaiwa kukaribia kumsajili
mshambuliaji wa Manchester City Wilfried Bony.
Bony aliwasili katika uwanja wa mazoezi wa Stoke
mapema leo ikiwa ni mchakato wa kukamilisha uhamisho wake kabla ya kufungwa kwa
dirisha la
usajili, ingawa klabu hizo mbili zinadaiwa bado kufikia muafaka wa
mwisho.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast bado
hajacheza katika mechi yeyote msimu huu na City wamekuwa wakimtafutia klabu
mpya katika wiki za karibuni.
Post a Comment