
TIMU ya Taifa ya soka la wanawake ya Tanzania Twiga
Stars imepangwa Kundi B pamoja na Ethiopia na Rwanda katika michuano ya ubingwa
wa wanawake kwa mataifa ya Afrika Mashariki na Kati.
Msemaji Mkuu wa TFF Alfred Lucas amesema kuwa utambulisho
wa michuano hiyo ya Challenge kwa upande wa wanawake ilifanyika jana mjini
kampala, wenyeji wa michuano iyo watakuwa ni nchi ya Uganda.
Amesema timu hiyo itakuwa na kambi yake katika
Hosteli za karume kwa muda wa wiki moja kabla ya kufanya kambi ya muda mrefu
kujiandaa na michuano hiyo.
Mbali za Tanzania, Ethiopia na Rwanda Kundi A
linaundwa na timu za Uganda, Kenya, Burundi, na Zanzibar na michuano itaanza
Septemba 11 hadi 20, 2016.
Kwa upande mwingine Lucas ameelezea kuendelea kwa
timu ya Taifa Stars na mazoezi yake wakijiweka sawa kwa ajili ya mchezoi wake
dhidi ya timu ya Nigeri utakaopigwa Septemba 3 mwaka huu.
Lucas hakuishia hapo ameelezea pia kuingia kambini
kwa timu ya Tifa ya vija ya Serengeti Boys ambayo inatarajiwa kuingia kambini
jumatano hii kabla haijaelekea nchini Shelisheli kwa ajili ya kuweka kambi ya
muda mrefu zaidi.
Post a Comment