
Kocha Pep Guardiola amesema kuwa klabu yake ya Manchester
City itafanya kila iwezavyo kuhakikisha watamtafutia klabu mpya kipa wao Joe
Hart.
Baada ya ujio wa kipya mpya ndani ya klabu hiyo
Claudio Bravo’s, Hart yupo huru kuondoka klabuni hapo na klabu za Sevilla na
Everton zimeonyesha nia ya kumuwania kipa huyo.
Guardiola amesema wanahitaji kupata klabu ambayo
itakuwa na msaada kipa huyo kwa ajili ya maisha yake ya baadae na klabu yao
itamsaidia kutafuta klabu nyingine kwa ajili ya kulinda kipaji chake.
Post a Comment