
MLINDA mlango wa Manchester City, Joe Hart amesema kuisaidia
timu hiyo kutinga hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika
mchezo ambao unaweza kuwa wa mwisho kwake kuitumikia klabu hiyo, ni jambo ya
kipekee.
Akihojiwa mara baada ya mchezo huo ambao City
walizonga mbele kwa jumla ya mabao 6-0, Hart amesema wana meneja bora ambaye
atakuwa na mawazo tofauti katika maamuzi yake.
Hart ambaye anategemewa kuondoka kufuatia Claudio
Bravo kukaribia kukamilisha usajili wake, alikuwa akipigiwa kelele na mashabiki
wakati wote wa mchezo huo wa marudiano ambao City ilishinda bao 1-0 dhidi ya
Steaua Bucharest.
Post a Comment