
MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa
Tanzania, Mbwana Samatta leo anatarajiwa kuingoza klabu yake ya KRC Genk ya
Ubelgiji katika mchezo wa marudiano wa mwisho kuwania nafasi ya kufuzu hatua ya
makundi ya michuano ya Europa League dhidi ya Lokomotiva Zagreb ya Croatia.
Katika mchezo huo Genk watakuwa
katika Uwanja wao wa nyumbani wa Luminus Arena wakijaribu kutafuta matokeo ya
kusonga mbele baada ya sare ya mabao 2-2 katika mchezo wao wa mkondo wa kwanza
uliochezwa katika Uwanja wa Maksimir jijini Zagreb.
Katika mchezo uliopita Samatta
ambaye pia ni nahodha wa Taifa Stars, alifunga bao katika sare hiyo
iliyopatikana na wanakwenda katika mchezo huo wakiwa wametoka kushinda mchezo
wao ligi ya Ubelgiji kwa mabao 3-0 Jumapili iliyopita huku Samatta akifunga
mabao mawili kati ya hayo.
Post a Comment