Halloween Costume ideas 2015

TANGAZA NASI.

TANGAZA NASI.

KESHO TANZANIA WATACHOMOKA KWA WAIVORY COST BEACH SOCCER?.



Image result for BEACH SOKA TANZANIA 
Timu ya Taifa ya soka la ufukweni Beach Soccer ijumaa hii inatarajia kushuka dimbani kukipiga dhidi ya Ivory Cost katika mchezo wao wa kusaka tiketi ya kufuzu kucheza fainali za kombe la mataifa ya Afrika.

Mchezo huo utachezeshwa na waamuzi kutoka Uganda ambao ni Shafic Mugerwa katikati na wasaidizi wake ni Ivan Bayige Kintu na Muhammad Ssenteza.

Mtunza muda katika mchezo huo atakuwa Adil Ouchker wa Morocco huku Kamishna akiwa ni Reverien Ndikuriyo wa Burundi.

Timu hizo zinatarajiwa kucheza mechi mbili ambako mara baada ya mchezo wa Dar es Salaam, utarudiwa mwingine huko Ivory Coast na mshindi wa jumla atakuwa amefanikiwa kufuzu kwa fainali.

Kikosi hicho kinaunda  na wachezaji Talib Ame, Ahamada,  Mohammed Makame, Ahamed Rajab (golikipa) Khamis Said na Yacob Mohamed wote kutoka Zanzibar.

Wengine ni Ally Raby, Mwalimu Akida, Khalifa Mgaya, Rolland Revocatus, Juma Sultan, Rajab Ghana, Samwel Salonge, Kashiru Salum, Juma Juma na Kevin Baraka.

Post a Comment

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget