
SAKATA la beki Hassan Kessy limeendelea kuvuta hisia
za wadau wengi wa soka hapa nchini baada ya Kamati ya katiba,Sheria na Hadhi za
Wachezaji kusogeza mbele tarehe za kusikiliza kesi yake hadi Septemba 4 mwaka
huu.
Kesi hiyo imesogezwa mbele kutoka na wajumbe wa
Klabu ya soka ya Yanga kutotokea katika kikao ambacho kamati hiyo iliketi
kujadili sakata lao hilo huku wajumbe hao wakitakiwa kuwepo katika kikao
kilichofanyika Jumatatu hii.
Alfred Lucas msemaji wa TFF amesema wataiandikia
barua klabu ya Yanga kwa ajili ya kuhudhuria katika kikao hicho
kitakachofanyika Septemba 4 mwaka huu.
Post a Comment