Maandalizi ya mchezo wa kukata na shoka wa watani wa
jadi kati ya klabu ya soka ya Simba dhidi ya Yanga yameendelea kushika kasi
huku tiketi za mchezo huo zikitamzamiwa kuanza kuuzwa Jumatano hii katika vituo
mbalimbali hapa nchini.
Mchezo huo wa mzunguko wa Sita unatarajiwa kupigwa
katika dimba la uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Jumamosii huku Afrika
Mashariki ikitazamiwa kusimama kwa muda kutokana na uzito wa mchezo wenyewe.
Afisa habari wa Shirikisho la soka nchini Tanzania
TFF ALFRED LUCAS amesema kuwa wameanza kuuza tiketi hizo mapema kutokana na kuwapa
fursa watanzania kuweza kununua tiketi zao mapema ukizingati mchezo huo utaanza
kwa kutumia tiketi za mfumo wa Eletroniki.
Naye Galus Lyeta ambaye ni Meneja miraji wa kampuni
ya Selcom alikuwa na haya ya kuelekezea kuhusu matumizi ya mfumo huo kuelekea
katika mchezo huo wa watani wa jadi.
Kiingilio cha chini katika mchezo huo kitakuwa ni Sh. 7000 kwa viti vya kwaidia VIP A 30,000 VIP B 20,000
Post a Comment