Klabu ya soka ya Azam FC imerejea jijini Dra es
Salaam tayari kujiandaa tena na mchezo unaofata wa ligi kuu soka Tanzania bara
baada ya kutoka Mkoani Mtwara.
Azama FC ilikuwa Mtwara kucheza mchezo wake dhidi ya
Ndanda Fc huku ikishuhudiwa Azam ikikubali kipigo cha mabao 2-1 na kuendeleza
rekodi mbovu tangu ligi hiyo iianze.
Afisa habari wa Azam Fc
Jafary Idd amesema kilichotokea Mtwara ni sehemu ya mchezo tu kwa upande wao na
kuwataka mashabiki kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho kocha mkuu wa
timu hiyo anayafanyika kazi makosa madogo madogo ndani ya klabu yao.
Post a Comment