HALI YA AFYA YA FURY YAHARISHA PAMBANO LAKE.
Mapromota wake hawakufichua taarifa zaidi lakini wamesema " hali yake ni mbaya mno na haimruhusu kushiriki pambano hilo".
Fury, mwenye umri wa miaka 28, alimshinda Klitschko kutoka Ukraine kwa pointi katika pambano la kwanza mnamo Novemba mwaka jana.
Pambano la awali lilipangwa Julai 9 katika uwanja wa Manchester Arena, na liliahirishwa hadi Juni baada ya Fury kuvunja fupa la kisigino chake.
Pambano jipya la kati ya mabondia hayo wawili liliangwa kufanyika Octoba 29.
Post a Comment