Kocha Arsene Wenger atakuwa katika harakati za kufuta uteja wa kufungwa na na klabu ya soka ya Chelsea leo hii katika mchezo wao wa Ligi kuu soka nchini Uingereza.
Wiki hii Arsene Wenger anasherehekea kutimiza miaka 20 tangu alipotangazwa kuwa meneja wa Arsenal, atakabiliana na timu ambayo amekuwa na uhasama nayo kwa muda mrefu.
Mfaransa huyo anatumai kuweka kumbukumbu yake ya miaka 20 kwa ushindi lakini timu yake imeshindwa kupata ushindi dhidi ya Chelsea katika mechi tisa walizokutana Ligi Kuu Uingereza na miamba hao wa Darajani Stamford.
Kwa hakika, Arsenal pia wameshindwa kufunga katika mechi zao sita za mwisho za ligi dhidi ya Chelsea lakini ushindi hapa unaweza kuwapa ushindi wa nne mfululizo wa ligi kwa mara ya kwanza tangu Oktoba.
Conte ndiye atakayesimama kidete kushindana na Wenger, akiwa anataka kukwepa kupoteza mechi ya tatu ya Ligi Kuu kwa mara ya kwanza tangu alipopata sare nne mfululizo akiwa na Juventus Machi 2012.
Post a Comment