KLABU ya soka ya Ruvu Shooting imeibuka na kuendelea
kupigilia msumari wa moto juu ya maamuzi mabaya ya waamuzi wanaochezesha
michezo ya ligi kuu soka Tanzania bara kwa msimu huu na kudai kuwa yanazigharimu
timu zao.
Afisa habari wa Ruvu
Shooting Masau Bwire amesema kuwa kuchezesha mpira bila kutambua sheria 17 za
mchezo wa soka kunaathari kubwa sana kwa vilabu husika lakini pia kunauwezekano
wa kushusha viwango vya timu husika.
BWIRE amesema kuwa mbali na kuwalaumu waaamuzi
lakini pia ameviomba vilabu nchini kuhakikisha wanapata nafasi ya kuweza
kujikubusha juu ya kusoma na kuelewa kanuni za mchezo wa soka ili kuondoa
makele ya kuwalaumu waamuzi hata kama wapo sahihi.
Post a Comment