Baada ya kutwaa kombe la Mataifa ya Afrika na Kati kocha
mkuu wa timu ya wanawake ya Kilimanjaro Queens Sebastian Nkoma amesema kuwa
kunakila sababu ya kuiandaa timu ya Taifa soka la wanawake Twiga Stars kupitia
timu hiyo baada ya kutwaa kombe hilo la michuano ya Challenge kwa upande wa
wanawake.
Nkoma amesema kuwa kukijenga kikosi cha timu hiyo
kunategemea na na mandalizi yatakayofanyika katika ligi ya wanawake
inayotarajiwa kuanza hivi karibu hapa nchini.
Amesema mbali na kukiandaa kikosi hicho lakini
amewasilisha ripoti yake katika ofisi ya TFF kwa ajili kupata nafasi ya kuandaa
timu hiyo kwa michuano mbali mbali ijayo.
Post a Comment