KIKOSI cha Mbeya fc
kinatarajia kushuka kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya hapo
kesho(Ijumaa) kucheza mchezo mwingine muhimu wa ligi kuu ya soka Tanzania bara
dhidi ya wageni Stand United kutoka
mkoani Shinyanga kikiwa bila nyota wake kadhaa wa safu ya ulinzi.
Kwa mujibu wa
Ofisa habari, Dismas Ten, maandalizi
kuelekea mchezo huo yamekamiliki na City
itashuka dimbani ikiendelea kuwakosa nyota wake wawili wa safu ya ulinzi,
Haruna Shamte na Sankhani Mkandawile ambao walimua kwenye mchezo wa ugenini dhidi ya JKT Ruvu uliochezwa Mlandizi mkoani Pwani na City
kufungwa bao 2-0.
Katika
Hatua nyingine nahodha wa Mbeya
City Fc , Kenny Ally ameipogeza timu ya taifa ya vijana Serengeti Boys kwa
hatua nzuri waliyofikia licha ya kushindwa kufuzu kwa michuano ya Afrika baada
ya kufungwa bao la dakika za lala salama
kwenye mchezo wao wa mwisho huko nchini Congo.
Kenny Ally ambaye alikuwa mmoja wa nyota wa timu ya
taifa ya Tanzania waliokwenda nchini Brazil na kutwaa kombe la Copa Coca cola
licha ya kutoa pongezi wa shirikisho pia alitoa wito kwa rais Jamal Malinzi
kuhakikisha anaitunza vyema timu hii ili ije kuwa timu nzuri ya taifa siku za
usoni.
Post a Comment