Klabu ya soka ya Simba imemuomba radhi rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania dkt. John Pombe Magufuli kupitia wizara ya
habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo baada ya mashakiki wa klabu hiyo kufanya
uharibifu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari katika makao Makuu ya klabu hiyo Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano cha klabu ya soka
ya Simba Hajji Manara amesema
kilichofanywa na mashabiki wao wanakilaani vikari na kuomba radhi wa rais
Magufuli kwa kitendo hicho.
MANARA pia ametaja kamati mpya mashindano ya klabu
hiyo kwa msimu huu mpya ligi kuu soka Tanzania bara nakueleza kupendezwa na
ufanyaji kazi wa watu waliopo kwenye kamati hiyo.
Post a Comment