Kamati ya kimataifa ya Olimpiki OIC imelaumiwa kwa
kushindwa kuhakikisha wanariadha walioshiriki michuano ya Rio mwaka huu
walikuwa hawatumii dawa zilizokataliwa michezoni.
Taarifa ya wakala wa kupambana na dawa hizo
ulimwenguni WADA imesema OIC ilianza kupoteza mwelekeo kabla hata ya michuano
hiyo kuanza.
Taarifa hii imekuja baada ya OIC kuifungia Urusi na
kisha kuifungulia kushiriki michuano ya Rio huku WADA wakiamini hawakustahili
kufanya hivyo.
Zaidi ya wanaridha 270 wa Urusi waliruhusiwa
kushiriki michuano hiyo baada ya kukata rufaa.
Hata hivyo kamati ya kimataifa ya Paralimpiki (IPC)
iliwazuia wanamichezo wa Urusi kushiriki michuano ya Rio 2016.
Post a Comment