Klabu ya soka ya Simba imepanga kuondoka mapema
jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wake dhidi ya Tanzania
Prison mapema wiki ijayo.
Akizungumza na waandishi wa habari Afisa habari wa
klabu ya simba Hajji Manara amesema kuwa wanasubiri taarifa kutoka kwa kocha
wao Joseph Omog kuona jinsi gani wanaweza kuondoka.
Katika mechi saba zilizopita, Simba imeshinda tano
na kutoka sare mbili hivyo kuifanya iendelee kukaa kileleni ikiwa imejikusanyia
pointi 17 kibindoni na kufanya izidi kuongoza Ligi Kuu soka Tanzania Bara na
sasa kinaanza rasmi kucheza mechi za mikoani.
Post a Comment