Nyota wa kimataifa wa Ureno, Cristiano
Ronaldo amesema amefurahi kuanza tena kuisaidia timu hiyo baada ya kufunga
mabao manne katika ushindi wa mabao 6-0 waliopata dhidi ya Andorra jana.
Akihojiwa Ronaldo amesema walifahamu kuwa bao la
kuongoza lilikuwa muhimu kwa timu hiyo ambayo ilikuwa ikijihami sana hivyo
amefurahi kufanikisha hilo na kupelekea kupata ushindi mnono.
Mabao hayo manne aliyofunga Ronaldo yamemfanya
kufikisha mabao 65 katika mechi za kimataifa na anaweza kuongeza mengine zaidi
wakati watakapovaana na Visiwa vya Faroe kesho kutwa kwenye mchezo mwingine wa
kundi B.
Post a Comment