KOCHA wa Real Madrid, Zinedine Zidane amesema hawezi
kuwa kocha wa Paris Saint-Germain-PSG kwani itakuwa kinyume kutokana na mapenzi
makubwa aliyonayo kwa timu ya nyumbani kwao ya Olympique Marseille.
Zidane ambaye aliiongoza Madrid kutwaa taji lao la
11 la michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita, amesema anafahamu kuwa
ipo siku atatimuliwa na klabu hiyo.
Kiungo huyo wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa
mwenye umri wa miaka 44, amesema kuinoa Marseille ni jambo ambalo siku moja
linaweza kutokea lakini kuifundisha PSG haitawezekana.
Post a Comment