Magoli la kipindi cha kwanza yaliyofungwa na Julian
Draxler na Sami Khedira yalitosha kuipa ushindi timu ya Ujerumani walipocheza na Northern
Ireland katika mchezo wa kuwania kufuzu kombe la dunia mwaka 2018.
Draxler alifunga goli lake la kwanza mnamo dakika ya 13 ya
mchezo akipiga mpira mzuri uliojaa wavuni akiwa katika kilinge cha kupigia
kona.
Huku Khedira akifunga bao lake la pili baada ya dakika 4
baadae baada ya Mats Hummels kuangushwa karibu na lango la goli.
Northern Ireland wapo katika nafasi ya tatu katika
kundi lao wakiwa wanaalama 4 wakati Ujerumani wakiwa wanaongoza kundi lao baada
ya kushinda michezo mitatu.
Post a Comment