LIGI Kuu soka Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa
kuendelea kesho Jumatano Oktoba 12, 2016 kwa michezo saba huku ule mchezo kati
ya Young Africans ya Dar es Salaam dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro ukipangwa
kufanyika Uwanja wa Uhuru jijini.
Michezo mingine itakayopigwa Jumatano ni kati ya
Mbeya City ya Mbeya na Simba ya Dar es Salaam, mechi itakayopigwa kwenye Uwanja
wa Sokoine jijini Mbeya.
Majimaji itaikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa
Majimaji mjini Songea wakati JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons kwenye
Uwanja wa Mabatini, Pwani.
Stand United itaikaribisha Azam FC kwenye Uwanja wa
CCM Kambarage mjini Shinyanga na katika mkoa huo huo Mwadui itakuwa mwenyeji wa
African Lyon kwenye dimba la Mwadui Complex.
Timu pinzani
za Mwanza ‘Mwanza Derby’ kati ya Mbao na Toto Africans itapigwa Uwanja wa CCM
Kirumba jijini humo.
Alhamisi
Oktoba 13, 2016
Ruvu Shooting itacheza na Ndanda FC kwenye Uwanja wa
Mabatini.
Post a Comment