Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF limesema kuwa
halitambua mkataba uliosainiwa na klabu ya Yanga kuhusu kukodishwa kwake na
kuiandikia barua klabu hiyo kupelekea nakala ya kopi ya mkataba huo.
Akizungumza na waandishi wa habari Katibu Mkuu wa
TFF Selestine Mwesigwa amesema kuwa klabu hiyo wameiandikia barua ili
kupewa nakala ya mkataba huo na kuona ni namna gani klabu hiyo itakuwa
ikiendeshwa.
Mwesegwa amesema kuwa kumekuwa na minong’ono mingi
kuhusu umilikiwa wa klabu hiyo na kupokea malalamiko kutoka kwa wazee wa klabu
hiyo kutoridhishwa na naamna klabu hiyo itakavyoendeshwa.
Post a Comment