Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Charles
Boniface Mkwasa amesema anaamini ziara za kusaka vipaji vipya mikoani zitasaidia
kukidhi hitaji la kuwa na wachezaji watakaounda kikosi bora.
Mkwasa amesema hatobagua wachezaji kwa kuzingatia
ligi kuu ama ligi daraja la kwanza, bali atafanya kazi hiyo kwa uwezo na wigo
mpana wa kuwafuatilia wachezaji wenye vigezo anavyo vihitaji.
Amesema kwa siku ya leo anaendelea na ziara ya kutafuta vipaji katika mchezo wa Yanga na Mtibwa kabla ya kuondoka siku ya Kesho kuelekea kibaha kutazama mchezomwingine wa ligi kuu.
Post a Comment