Katibu mkuu wa Baraza La Michezo La Taifa BMT
Mohamed Kiganja amesema hana shaka na suala la baraza hilo kufikishwa katika
vyombo vya kisheria,kufuatia sakata luililoibuka siku za hivi karibuni la
kukabidhi majukumu ya usimamizi wa mchezo wa ngumi za kulipwa kuwa chini ya
kamisheni ya numi za kulipwa nchini TPBC.
Kiganja amesema anafahamu kampuni zinazoendesha
shughuli za mchezo huo TPBO, PTS pamoja na TPBC Limited vimebisha hodi mahakama
kuu kanda ya Dar es salaam, kwa lengo la kusaka tafsiri ya kufahamu kama BMT
wana mamlaka ya kuwapa TPBC usimamizi wa ngumi za kulipwa.
Amesema suala hilo limefanyiwa maamuzi na BMT kwa
maslahi ya wadau wote wa mchezo wa ngumi za kulipwa, lakinia naloliona kwa sasa
ni baadhi ya watu kutetea maslahi yao kwanza na kuwasahau wengine ambao wamekua
wakivuja jasho ulingoni.
Post a Comment