Shirikisho la soka nchini TFF limesema zoezi la
kufuatilia suala la umri wa mchezaji wa timu ya taifa ya vijana ya Congo
Brazzavile LANGA LESSE bado linaendelea.
Mchezaji huyo ambaye anadaiwa kuwa na umri mkubwa,
hivi karibuni alishiriki mashindano ya kusaka tiketi ya kushiriki fainali za
Afrika za vijana wenye miaka chini ya 17.
Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF ALFRED LUCAS
amesema suala hilo hawawezi kulizembea kwasababu ni kubwa na lina vitu vingi
vya utata ikiwemo kitendo cha mchezaji huyo kuvaa jezi zinye namba tofauti
katika kila mechi za kimataifa alizokuwa anacheza.
Post a Comment