Klabu ya soka ya Arsenal imeanza kumnyatia mlinda
mlango wa klabu ya soka ya Atletico Madrid Jan Oblak kuweza kumsajili kuchukua
nafasi ya Petr Cech’s.
Mchezaji huyo mwenye miaka 23ameonyesha kiwango
kizuri katika viunga vya klabu hiyo ya nchini Hispani Vicente Calderon na
amekuwa mmoja wa makipa bora zaidi barani Ulaya.
Lakini klabu hiyo imeweka bayana kuwa ipo tayari
kupokea ofa ya klabu yoyote itakayojitokeza kumsajili mchezaji huyo huku
ikionyesha wazi kuwa klabu ya Arsenal ikifunguliwa milango ya kumtwa mlinda
mlango huyo kwa dau la €100million .
Post a Comment