Klabu ya Manchester United itacheza dhidi ya Hull
City katika nusu fainali ya Kombe la ligi ya Uingereza EFL ,huku Liverpool
ikipepetana na Southampton.
United ambayo iliishinda West Ham 4-1 katika robo
fainali watacheza mechi ya kwanza dhidi ya Hull City katika uwanja wa Old
Trafford.
Southampton ,ambayo iliishinda Arsenal kwa urahisi
siku ya Jumatano itaialika nyumbani Liverpool katika uwanja wa St. Mary kabla
ya mechi ya marudiano itakayochezwa katika uwanja wa Anfield.
Mechi hizo zitachezwa tarehe 9 na 23 mwezi Januari
2017.
Liverpool ambao ni washindi wa kombe hilo kwa mara
ya nane na kuwahi kufuzu katika fainali 2016, iliishinda Leeds United siku ya
Jumanne.
Hull, ambao walifika fainali ya FA mwaka 2014,
ilihitaji penalti kuwashinda Newcastle siku ya Jumanne.
Post a Comment