
Na Merina Robert
Morogoro
KESI ya tuhuma ya kutoa rushwa ya chakula cha
shilingi milioni moja kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa chama cha soka manispaa ya
Morogoro(MMFA) ili waweze kumchagua inayomkabili katibu wa
chama hicho Kafale Maharagande inatarajia kuanza kusikilizwa Septemba
kumi na tano mwaka huu baada ya taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa(TAKUKURU) kuiambia mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro kwamba
upelelezi umekamilika.
Kwa mujibu wa mwendesha mashitaka wa TAKUKURU mkoa
wa Morogoro Cleoce Cleophace aliambia mahakama kuwa mashihidi kumi na mbili wanatarajia kutoa
ushahidi kuhusiana na kesi hiyo mahakamani hapo ambapo pia vielelezo vinne vitawasilishwa .
Kafale
Maharagande anashitakiwa kwa tuhuma ya
kutoa rushwa Julai ishirini na
nne mwaka huu katika ukumbi wa manispaa
ya Morogoro akiwa mgombea wa nafasi ya Katibu wa MMFA kushawishi wajumbe wa
mkutano mkuu wa chama hicho kwa kutoa
chakula cha shilingi milioni moja ili waweze kumchagua katika nafasi aliyokuwa
akiigombe.
Akisoma shitaka
mbele ya hakimu mkazi wa Mkoa wa Morogoro Ivan Msaki ,mwendesha
mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) mkoa wa
Morogoro Cleonce Cleophace alidai kuwa
hatua ya mshitakiwa kutoa rushwa ya chakula kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa MMFA ni
kinyume na kifungu cha kumi na tano cha
sharia ya Kuzuia na Kupambana na rushwa
ya mwaka elfu mbili na saba.
Hata hivyo mshitakiwa alikana shitaka lenye
vipengele tisa ambavyo kati ya hivyo nane alivikubali huku kipengele kimoja
akikana na kwamba mshitakiwa yupo nje kwa dhamana hadi Septembe kumi na tano
kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.