Na Nicolaus Kilowoko
Muimbaji siku zote ni mburudishaji wa nafsi za watu na
kuwafanya watu waburudike kwa kusikiliza muziki mzuri ambao unaambatana na
vionjo mbalimbali vya muziki ikiwemo viombo vya muziki huo lakini pia hata
sauti ya Muimbaji huyo.
Muimbaji unaweza kuimba kutokana na kuirushusu misuli
yako vyema lakini pia kutoa sauti iliyo bora zaidi kutoka kinywani na kufanya
sauti yako kuwa na mvuto wa aina yake.
Waimbaji wengi wamekuwa wakitengeneza sauti zao kwa
kuimba sehemu zilizo wazi,kukimbia,lakini wengine wakifanya mazoezi ya kupiga
push up,huku wengine wakila vyakula ambavyo vimekuwa haviwasaidii sana.
Siku zote tumekuwa tukiwafahamu waimbaji mbalimbali lakini
leo hebu tujaribu kuona ni jinsi gani muimbaji anaweza kuwa na sauti nzuri na
kuweza kuendelea kuwaburudisha mashabiki wake kwa kuzingatia vyakula
vifauatavyo.
Kwa kujali miili ya waimbaji lazima utambue mwili wako
lazima ujengwe kwa chakula bora na kuna vyakula ambayo muimbaji unapaswa
kuvizingatia kuhakikisha hauvitumii na kuna vyakula ambavyo unapaswa uvitumie
ili kuweza kuilinda sauti yako kuwa nzuri na kuendelea kuwaburudisha mashabiki
wao.
Vyakula ambayo muimbaji unapswa kula kabla
ya kutumbuiza.
Kuna vyakula ambavyo unaweza ukavifurahia kula kabla
ya kufanya onyesho lako na kuifanya sauti yako iwe nzuri na yenye mvuto zaidi
lakini pia haipaswi ule kupita kiasi.
Siku zote muimbaji unapaswa kuangalia na kuweka uwiano
wa vyakula hivi wakati wa kula kwa kuzingati kuimarisha mwili lakini kuifanya
sauti yako pia kuwa nzuri na hata nguvu mwilini.
Kuna vyakula ambayo unatakiwa uvitumie kwa wakati wote
kwa kuimarisha sauti yako kwa kuchagua matunda ambayo ni mazuri kuliko kunywa
juisi kutokana na kuwa yanaenda moja kwa moja katika mfumo wako wa damu na
kufanya damu kutembea kwa haraka na kuifanya sauti yako itoke yenye uharisia.
Chakula kama nyama ya kuku kwanza inaongeza protini
nyingi mwilini na kumfanya muimbaji kupata nguvu ambayo inayokufanya utoe sauti
iliyokuwa na nguvu ya kutosha pasipo kubanwa.
Nyama ya samaki kama ambavyo
ilivyo kwa nyama ya kuku pia inaongeza protini mwilini, kwa kuipika vyema pasipo
kuikosea itakufanya utoe sauti nzuri.
Vyakula vyenye vitamin kama Vitamin
A ikiwemo nyama ya ng’ombe lakini pia kutumia mayai,matunda mfano
maembe,matikiti maji,mapeasi na viazi
vya njano.
Karanga pia ni moja ya chakula
ambacho kinaweza kukufanya kama muimbaji uweze kuwa na sauti nzuri wakati wa
kuimba.
Mbali na kutumia vyakula
vyote hivi lakini pia muimbaji unapaswa kunywa maji ya moto kwa wingi na
kufanya sauti yako kuendelea kuwa imara zaidi.
Lakini pia maji hayo unaweza
kuchanganya pia na asali na ukanywa na kwa mchanganyo huo unaweza ukabadirisha
sehemu kubwa ya sauti yako na kuwa ya mvuto kwa uimbaji wa aina yoyote.
Unywaji huu wa mchanganyiko
wa asali na maji unaweza ukanywa siku moja kabla ya onyesho lako na kuweza
kuitengeneza sauti yako kuwa yenye utofauti wa siku zote.
Vyakula ambavyo muimbaji hupaswi kuvitumia
kabla ya kutumbuiza.
Tunajua kuwa kila chakula kina utamu wake pindi
utumiapo lakini kunavyakula muimbaji hupaswi kuvitumia wakati unajiaandaa
kutumbuiza mbele ya mashabiki wako kwakua vianaweza kusababisha kuharibu sauti
yako.
Maziwa tunajua ni matamu kwa mnywaji lakini kwa muimbaji
hupaswi kutumia kabla ya kuelekea kwenye kutumbuiza kutokana na kuwa yanaongeza
Acid ambayo inaweza kukusababishia ukashindwa kutoa sauti iliyob ora zaidi.
Mbali na maziwa pia vyakula vyenye sukari unapaswa
uviache kabla ya kuanza kutumbuiza mfano juisi iliyochanganywa na sukari
kutokana na kuwa inatengeneza mabaki mabaki ndani ya kinywa chako yanayoweza
kukusababishia ushindwe kutoa sauti kwa wakati na ikakusababishia sauti kukwama
kwama.
Kitu kingine ni kahawa
haupswi kuitumi kabla ya kufanya onyesho lako kutokana na kuwa sauti yako
inapaswa kutoka kwa uzuri zaidi ili kuweza kuimba kwa ufasaha lakini utumiapo
kahawa inatengeneza kubanwa kwa sauti yako.
Mbali na kahawa kitu kingine
ambacho ni muimbaji hupaswi kuvitumia ni pamoja na
soda,pilipili,chocolate,pombe ya aina yoyote na vitu kama hivyo.
Post a Comment
Ahsante sana ndg ila vp kuhusu mayai mabichi?
asante sana kwa ushauri huu juu ya uimbaji na vyakula vya kutumia maana wengi wetu hatufahamu zaidi
asante sana kwa ushauri huu juu ya uimbaji na vyakula vya kutumia maana wengi wetu hatufahamu zaidi
Asante sana ndugu
Thanks I get something
Somo nimelipendaa
Thanks for aidia
Ubarikiwe sana kwa ushaur na mafunzo mazur
Jamani mayai mabichi,kuna utafiti unaonyesha kua yana madhara makubwa kiafya,,
1: husababisha kuchanika kwa ulimi (madonda kwenye ulimi) kutokana na kemikali iliyoko kwenye ute mweupe wa yai,,
2.kuna bacteria hupenda kua either ndani ya yai au nje kwenye ganda lake , bacteria huyu anaitwa salmonella, yeye hupelekea kuharisha masaa 72 baada ya kutumia yai,pia maumivu makali ya tumbo,...
Asante sana kwa ushauri.mafunzo tumepata elimu kubwa
Nashukur kwa somo
Thank You So Much Mzee Baba Nimepata Vema Ushauri
🙏🙏 Asante sana
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.