Msimu wa majira ya joto hauwezi kupita bila ya James Rodriguez, Gareth Bale na Neymar kujaribu kuondoka katika klabu kubwa mbili za Hispania kutua Manchester United kucheza na Phil Jones.
Mapema juma hili, habari zimesambaa kuwa uhamisho wa Rodriguez kwenda Old Trafford utathibitika Jumapili na kwamba Gareth Bale, kupitia wawakilishi wake ameweka bayana kuwa anataka kuwa sehemu ya kikosi cha Jose Mourinho ikiwa ataondoka Real Madrid.
Sasa, kwa mujibu wa habari nyingine, Neymar naye anaweza kuwa kwenye mchakato wa kutua Manchester United pia.
Ripoti zinadai kuwa United wanataka kumleta nyota huyo Old Trafford kwani Jose Mourinho ataendelea kutumia fedha zaidi kuisuka Man United mpya na kuirejeshea hadhi yake Ulaya.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.