Mchezaji wa zamani wa Barcelona Xavi ameitahadharisha
Real Madrid kuwa Malaga si timu rahisi na kuifunga kwenye uwanja wao wa
nyumbani ni kazi ngumu.
Los Blancos sasa wanahitaji pointi moja tu kutwaa
ubingwa wa La Liga kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitano kuelekea mechi ya
Jumapili ugenini dhidi ya Malaga wakati Barcelona wakivaana na Eibar.
Madrid wanapewa nafasi kubwa kuifunga Malaga lakini
Xavi anaamini mechi hiyo itakuwa ngumu kutokana na kiwango safi cha timu ya
Michel ambayo imefungwa mechi moja tu katika nane za mwisho.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.