Na Nicolaus Kilowoko.
Osinach Kalu ni Mwanamuziki lakini pia ni mwandishi wa
nyimbo za injili aliyezaliwa nchini Nigeria akiwa ni mtoto wa pili kuzaliwa
kati ya watoto saba wa mzee Kalu.
Osinach amezea kuuteka muziki wa njili duniani na kuwa
moja kati ya wasii wanaopendwa zaidi na kumfanya awezae kubadirisha jina lake
hilo na kutunia jina jingine.
Osinach amekuwa akifahamika kwa jina hilo lakini
aliweza kubadirisha jina hilo la Osinachi na kuwa Sinach kutokana na yeye
mwenyewe kuona kuwa jina lake linashindikana
kutamkwa nyema na kuona Sinach linaweza kuwa ni raisi kwa watu kuweza kulishika
kirahisi na kuweza kulitamkika midomoni mwa mwao.
Mbali na muziki lakini pia Sinach alifanikiwa kufunga
ndoa na mumewe Joseph Egbu mnamo mwezi June mwaka 2014 katika kanisa la Ikeja, mjini
Lagos, nchini Nigeria.
Lakini pia Sinach mbali na kuwa muandishi wa nyimbo
zake pia ni kiongozi wa dini katika kanisa mabalo yeye anasali na kuendelea kuongeza
imani kwa watu kumuamini Mungu kwa kumsikiliza yeye kama kiongozi lakini pia
kwa kusikiliza nyimbo zake.
Sinach mbali na kufanya muziki lakini aliwahi kukiri
kukosa kuungwa mkono na baba yake ambaye hapendi mwanae afanye kazi hiyo ya
muziki huku mwenyewe akiamini kuwa muziki ni ndoto yake na unaweza kubadirisha
maisha ya watu kutokana na muziki.
Sinach ni mwanamuziki ambaye ameweza kuandika nyimbo
takribani 200 huku pia akiweza kushinda tuzo mbalimbali kutokana na ubora wa
kazi yake ya muziki.
Pamoja na kuwa ni nyota duniani lakini pia hata katika
kazi za kumuabudu Mungu na siku zote amekuwa akiandika nyimbo ambazo zinaweza
kuishi kizazi hadi kizazi na kuleta mabadiriko katika jamii.
Mnamo mwaka 2008 aliweza kushinda tuzo ya nyimbo bora
ya mwaka katika wimbo wake wa “This Is Your Season” mbali na kushinda tuzo hiyo
lakini nyimbo zake zimekuwa zikiibwa katika makanisa mbalimbali ulimwenguni na
kuzidi kumfanya afahamike zaidi.
Mbali na kushinda tuzo hizo lakini pia Sinach ameweza
kushinda tuzo za mwimbaji ambaye anaweza kusifu na kuabudi wakati akiwa
jukwaani ukiwemo mwaka 2007, 2008 na 2009.
Na kati ya wimbo ambao unapendwa ulimwenguni kote kwa
watoto na watu wazima ni ule wa “I Know Who I Am” alioutoa mwaka 2012 ambao
mpaka kesho bado hauchuji wala hauchoshi masikioni mwa mashabiki wake kutokana
na kugusa maisha yayao kwa asilimia kubwa.
Wimbo huu umekuwa ukitumika sana katika matukio
mbalimbali ya kumsifu na kumuabudu Mungu lakini pia umekuwa wimbo wa wenye
shida mbalimbali kuweza kujifariji wapatapo mataizo.
Umekuwa wimbo ambao wanachi wa Uganda na Kenya
wamezidi kuupenda kutokana na matatizo mbalimbali ambayo walishawahi kukutana
nayo hapo nyuma n ahata kumfanya yeye mwenyewe Sinach kufurahia kuona wimbo huu
unambeba zaaidi kati ya nyimbo zake zote.
Lakini mbali na kuweza kutumbuiza nchini Nigeria Sinach
ameweza kutumbuiza takribani nchi saba sasa ikiwemo nchi ya Kenya, katika
kanisa la Citam Karen, Afrika kusini, Marekani, Trinidad, Tobago, na nchini
Uganda katika kanisa la Miracle Centre Cathedral.
Sinach amekuwa mwanamuziki mwenye mafanikio zaidi
nchini Nigeria na kumfanya kuwa mwanamuziki bora wakati wote kutokana na ubora
wa nyimbo zake.
Ni mwanamuziki ambaye amekuwa na ndoto ya kubadirisha
mawazo ya watu tangu alipokuwa mdogo na ndio kitu ambacho anakifanya kwa sasa
kupitia nyimbo zake zenye ujumbe mzito wa kusisimua na zenye kufanya
zinawabadirisha watu kimtazamo.
Mbali na kufanya kazi ya kuimba lakini Sinach amekuwa
si mfanyabiashara katika nyimbo zake bali amekuwa mtu ambaye anawaza kuusogeza
muziki wa injili mbali na kufanya uwe ndio maisha ya watu.
Kitu ambacho kwa miaka ya hivi karibu imekuwa
ikiaminika kuwa muziki wa injili umekosa mvuto wake kutokana kuingiliwa na
wakati mwingine ukifananisha kama muziki wa dunia.
Umekuwa ukifananishwa kama muziki wa duniani baada ya
waimbaji wengi kufata mambo ya kidunia na kuyaingiza katika muziki huo na
kuufanya ukose radha ya kuwa muziki wa injili.
Jambo hilo ndilo linalomfanya Sinach kwa upande wake
kutotaka muziki wake kuwa kama biashara bali kuwa muziki ambao unaweza
ukawaokoa watu wengi na kubadirisha mitazamo yao ya maisha.
Amekuwa akiimba nyimbo zake kutoka moyoni na kutoa
nyimbo kutokana na maisha ya watu katika jamii husika na kutokata tamaa kwa
yale mambo magumu aliyowahi kuyapitia.
Amekuwa akisistiza kila mara anapoulizwa juu ya
wanamuziki ambao wamekuwa wakiimba muziki wa injili lakini ambao haunafaida
katika jamii hukua akisisitiza kuwa Mungu ndiyo kitu cha kwanza alafu
mwanamuziki ndiye anayefata.
Sinach amekuwa akitoa ushauri kila wakati kwa wanamuziki
wenzake kutokana na mafanikio yake akielezea kuwa muziki wake unakuwa kwa
kufanya maombi kwa Mungu hivyo wasitegemee wafadhiri katika kuwanyanyua
kimuziki.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.