Nyota wa klabu ya Arsenal, Olivier Giroud amesema
yeye pamoja na wachezaji wenzake wanapaswa kuongeza umakini pindi wawapo mbele
ya goli ili waweze kurejesha matumaini yao yam bio za ubingwa wa Ligi Kuu.
Kauli hiyo
imekuja kufuatia Arsenal jana kung’ang’aniwa sare ya bila kufungana na
Southampton na kuwafanya kuporomoka mpaka nafasi ya nne katika msimamo wa ligi
wakiwa alama tano nyuma ya vinara Leicester City.
Giroud amesema anafahamu safari bado ni ndefu lakini
wanahitaji kuongeza bidii pindi wanapofika katika lango la wapinzani ili waweze
kupata matokeo wanayohitaji.
Klabu ya Arsernal mchezo wao ujao watakutani dhidi
ya Bournemouth.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.