KOCHA wa Manchester United Louis van Gaal
ameipongeza klabu ya Manchester City kwa kumteua Pep Guardiola kuinoa timu hiyo
msimu ujao.
Akihojiwa mara baada ya ushindi wa mabao 3-0
waliopata dhidi ya Stoke City usiku wa kuamkia hii leo, Van Gaal amesema
Guardiola ni nahodha wake wa zamani hivyo atafurahi kukutana naye tena.
Van Gaal alikuwa meneja wa Guardiola wakati akiwa
Barcelona na ndio alimpa unahodha kiungo huyo wa zamani Camp Nou.
Guardiola raia wa Hispania toka wakati huo amekuwa
akifuata nyayo za bosi wake huyo wa zamani akiwa kama meneja na ufurahia
mafanikio makubwa wakati akizifundisha Barcelona na Bayern Munich.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.