Kikosi cha wachezaji 26 cha timu ya wanawake ya
Tanzania Kilimanjaro Queens kimetangazwa Alhamis hii kwa ajili ya kwenda nchini
Uganda kuwania nafasi ya kushiriki fainali za Michuano ya Kombe la Mataifa
Afrika Mashariki na Kati CECAFA kwa upande wa wanawake.
Akitaja kikosi hicho kocha mkuu wa timu hiyo
Sebastiani Nkomba amesema kikosi hichi cha wachezaji 26 hakijabadirika san
asana na kilichopita na amefata orodha ya wachezaji iliyoachwa na aliyekuwa
mwalimu wa timu hiyo Nasra Juma.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha soka la wanawake
nchini Tanzania Amina Karuma amesema kwa sasa wamejipanga vyema na soka la
wanawake nchini Tanzania na wanatarajiwa kuanzisha Ligi ya wanwake am,bayo
itahusisha Mikoa 9 ya nchini huku timu shiriki zikiwa ni 12.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.