Chelsea wamemrejesha beki wao kisiki David Luiz
waliomuuza miaka miwili iliyopita kwa Paris St- Germain, mchezaji huyu
kanunuliwa kwa kiasi cha pauni million 34. Pia Chelsea imemsajili Marcos Alonso
toka Fiorentina kwa pauni milion 23.
Moussa Sissoko amesajiliwa na Tottenham akitokea
Newcastle kwa pauni milioni 30, Leicester City wamesajili Islam Slimani toka Sporting
Lisbon kwa pauni 29.
Stoke City wamemsajili Wilfried Bony kwa mkopo toka
Manchester City, Samir Nasri nae amepelekwa kwa mkopo Sevilla toka kwa matajiri
wa Man City
Mshambuliaji Mario Balotelli wa Liverpool
amesajiliwa na Nice ya Ufaransa bure, West Ham wamsajili beki Alvaro Arbeloa
toka Real Madrid.
Valencia ya Hispania wamesamjili kwa mkopo wa muda
mrefu Eliaquim Mangala wa Manchester City, Nao Juventus wamemsajili Juan
Cuadrado kwa mkopo toka Chelsea kwa mkataba wa miaka mitatu.
Jack Wilshere ametua Bournemouth kwa mkopo wa msimu
mzima, Mshambuliaji Mkongo Dieumerci Mbokani asajiliwa na Hull City.
Enner
Valencia aenda Everton kwa mkopo hadi mwisho wa msimu kutoka West Ham.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.