Klabu ya soka ya Lipuli ya Mkoani Iringa inayoshiriki
Ligi Daraja la kwanza imejitamba kufanya vyema katika ligi hiyo inayotarajiwa
kuanza mapema Mwezi ujao.
Akizungumza na kituo hiki Mjumbe wa kamati ya
Utendaji ya klabu hiyo HARUNA SALEHE amesema kwa mazoezi wanayoendelea nayo
hivi sasa hanashaka yoyote juu ya klabu yake kutofanya vuzuri katika ligi hiyo
ambayo inaonekana kuwa na upinzani mkubwa kutokana na klabu zinazoshiriki ligi
hiyo.
Klabu hiyo ya Lipuli imeendelea na mazoezi yake
Jumatano hii katika uwanja wa Karume uliopo maeneo ya Karume jijini Dar es
Salaam kuyari kusubiri kupulizwa kwa kipyenga cha kuanza kwa ligi hiyo.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.