
Na Nicolaus Kilowoko
Tunapotaja waimbaji wa nyimbo
za injili ambao wamewahi kutamba katika tasnia ya Sanaa ya muziki ulimwenguni huwezi
kuacha kulitaja kundi la Makoma.
Makoma ni kundi la muziki wa
injili ambalo lilihusisha nyimbo za muziki wa maadhi ya rumba,pop na R&B ambalo
lilianzishwa mjini Kinshasa, katika nchi ya kidemokrasia ya Congo na kuweza
kukua zaidi nchini Uholanzi.
Kundi hili lilikuwa
linahusisha ndugu sita wakiwemo wakaka watatu na wadada watutu akiwemo Nathalie
Makoma, Annie Makoma, Pengani Makoma, Tutala Makoma, Duma Makoma, Martin Makoma
pamoja na rafiki yao mwingine alikuwa anajulikana kama Patrick Badine.
Kundi hili liliweza
kuitikisa sana dunia kipindi hicho cha miaka ya 2000 kwa nyimbo zao hasa kwa
wapenzi wa muziki wa injili na hata wale wanaosikiliza nyimbo za kidunia.
Kundi hili pia liweza kukua
zaidi baada ya kuanzishwa na Tutala Makoma mnamo mwaka 1993, na kuweza
kutumbuiza majukwaani kama kundi mwaka 1995 na wakati huo likijulikana kwa jina
la "Nouveau Testament".
Na siku zote waliweza
kutumia Lugha ya kilingala pamoja na kiingereza lakini pia waliweza kutumia
kifaransa,kiholanzi na Kijerumani kwa wakati mwingine.
Familia hii ilifanikiwa
kuondoka nchini Congo zamani ikijulikana kama Zaire kutokana na matatizo ya
kisiasa na waliweza kuelekea nchini Uholanzi ambapo baadae walielekea nchini
Ujerumani lakini baadae waliweza kurudi nchini Uholanzi mwaka 1996.
Wakati huo wakijulikana kama
“Nouveau Testament”The walifanikiwa kubadirisha jina hilo na kuamua kutumia
jina la familia lilojulikana kama Makoma na kuweza kukua zaidi barani Ulaya.
Makoma waliweza kufanikiwa
kurekodi katika studio ambazo zilikuwa zikimilikiwa na ndugu yao Tutala Makoma
huku kazi ya kuwaremba ndugu hao ikifanywa na Annie Makoma na Martin Makoma
aliweza kutengeneza mazingira mazuri ya picha na jukwaani.
Na albamu yao ya kwanza
kuitoa ilikuwa ni mwaka 2000 iliyojulikana kama “Nzambe Na Bomoyi” (jesus for
life), albam hii ndiyo iliyowapa umaarufu na kukamata tasnia ya muziki wa injili
ikitamba kwa nyimbo kama Napesi, Butu na moyi, Mwinda, Moto oyo, Natamboli ikifuatiwa
na albamu nyingine ya “On Faith” mwaka 2002.
Mwaka huo wa 2002 Makoma
walifanikiwa kushinda tuzo ya kundi bora kutoka barani Afrika zilizokuwa
zikisimamiwa na “Kora African Music Awards” na kuweza kuwafanya kuzunguka nchi
nyingi za barani Ulaya,Afrika na Canada.
Kundi la Makoma limeweza
kusaini katika lebo ya muziki ya “Media Limited, international record” huku Makao
Makuu yake yakiwa ni nchini Uingereza na Philipp Bauss akiwa ni Mkurugenzi wa
kampuni hiyo akiwa anazalisha kazi zote za video na nyimbo katika studio zake
mwenyewe.
Harakati za kundi hilo
hazikuishia hapo kwani mwaka huo huo wa 2002 walitoa albamu yao nyingine ya “Mokonzi
na Bakonzi” ikiwa na maana mfalme wa wafalme ikibeba nyimbo zilizoimbwa kwa
kilingala kama vile Nasengi,Bana, Naleli,Nzambe na Ngai na Tolingana.
Mwaka 2005 walifyatuan
albamu nyingine ya “Nzambe te” ikiwa na nyimbo kama Bomoyi te wakichanganya
Kilingala na kiingereza huku kundi hili lilitamba na kuwafanya kuendelea kuwa
juu katika muziki huko nchini uholanzi wakiimba bila ndugu yao Nathalie.
Kuvunjika kwa kundi la Makoma.
Kiongozi wa kundi hili
alikuwa ni Nathalie Makoma ambaye aliliacha kundi hili mnamo mwaka 2004 na
kuanza kuimba mwenyewe muziki wa kidunia na kufanya kazi za kuimba akiwa peke
yake na kuweza kutengeneza matamasha mwaka 2006.
Nathalie Makoma, alizaliwa
mnamo mwaka 1982 mjini Kinshasa na kufanikiwa kuwa mwimbaji mzuri sana nchini
Uholanzi na kuweza kufanikiwa kuachia nyimbo ka “On Faith”mwaka 2003 na “I Saw
the Light” mwaka 2005.
Nathalie alianza kuimba
mwaka 1993 katika bendi yao ilijulikana kama "Nouveau Testament"
kabla kujiunga na makoma alipofikisha miaka 14 alihamia uholanzi na kupata
elimu ya kulitawala jukwaa katika chuo cha rockacademie huko Tilburg.
Baada ya kundi la Makoma
kuzunguka duniani na kupata mafanikio nathalie aliacha shule rasmi na kuzunguka
na kundi hilo akitangaza injili kwa njia ya uimbaji.
Nathalie baada ya kulikacha
kundi hilo na kuamua kuimba muziki wa kidunia akiwa nje ya kanisa kutokana na
kile alichodai kutaka kufanya kazi nyingine, huku wajuzi wa mambo wakidaiwa
kuwa ni ugomvi baina yake na kaka yake mkubwa.
Mwaka 2007-2008, aliweza
kurudi nchini Uholanzi na kuweza kufanya kazi zake kule kabla ya baadae kuweza
kusaini mkataba na lebo ya Sony BMG.
Kurudi kwa Kundi la Makoma bila Nathaelie.
Kundi hili la Makoma liliweza
kurudi tena na kutengeneza albam yao mpya mnamo mwaka 2012 ambayo ilijulikana
kama Evolution ikihusisha nyimbo takribani 10.
Albamu ya Evolution
waliyoitoa ilikuwa na nyimbo kumi, kama vile Evolution, Alingi biso, Yo ozali,
Ndeko, Mokonzi, Se ye, Maboko Likolo, Mokili, Sosola na Nguya.
Albamu hiyo ambayo ni ya
kwanza tangu waungane imeweza kufanya vizuri kwenye vituo vya radio nchini kwao
walikozaliwa pamoja na nchini nyingine duniani bila kusahau Afrika ya Mashariki
na kati.
Na albamu yao ya tano ya My
sweet lord waliyofanya kama kundi waliweza kumshirikisha Nathalie kama mwimbaji
anayejitegemea.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.