Na Nicolaus Kilowoko.
Mwaka 2017 unaweza ukakumbukwa sana na wanasoka wengi
hasa bara la Afrika na kwa ulimwengu mzima baada ya kufanyika kwa michuano
yenye hari kubwa na mafanikio makubwa kwa timu shiriki katika michuano hiyo,
michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika “AFCON” au “CAN”.
Afcon ni michuano ambayo imegusa hisia za watu wengi
zaidi kwa mwaka huu wa 2017 kutokana na matukio yake toka kutangazwa kwa
mwenyeji wa michuano hiyo.
Kabla ya kufanyika nchini Gaboni michuano hiyo
ilitangazwa ingefanyika nchini Libya lakini mwaka 2014 kutokana na kuingia nchi
hiyo katika vita ya wenyewe kwa wenyewe ikaamua kujitoa uwenyeji wa michuano
hiyo.
Mchakato
wa mwenyeji wa michuano hiyo ulivyoanza.
Kwa mara ya kwanza mchakato huo ulikuwa na mvutano mkubwa
wa nani atakuwa mwenyeji wa michuano hiyo kutokana na nchi zenyewe zilizokuwa
zinaomba kuwa wenyeji.
Moja ya nchi ambazo zilikuwa katika mchakatao wa
kuomba uenyeji wa michuano hiyo ni pamoja na Botswana,Cameroon,DR
Congo,Guinea,Morocco,Afrika Kusini,Zambia,na Zimbabwe.
Katika mchakato huo Chama cha soka barani Afrika CAF kiliweza
kupata nchi tatu ambazo zilipatikana mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka 2010
ambapo zilichaguliwa nchi hizo kwaajili ya moja wapo angekuwa mwenyeji wa
michuano hiyo mwaka mwaka 2017.
Timu ambazo ziliingia katika kingang’anyiro mnamo
mwaka 2015 ni pamoja DR Congo, Morocco na Afrika Kusini.
Lakini CAF walianza kuchagua nchi ambayo inaweza kuwa
mwenyeji wa michuano hiyo kwa mara ya kwanza waliichagua nchi ya DR Congo kwa kuangalia
mazingira mbalimbali ya soka lakini badaye waliitoa baad ya DR Congo
kuwataarifu CAF kuwa wamejitoa katika kuandaa michuano hiyo kati ya mwaka 2015 na
2017.
Mchakato
wa pili kufanyika kupata mwenyeji wa michuano hiyo.
Baada ya hayo yote kufanyika na nchi zote kuwa haziko
tayari kuandaa na na nchi kama ya Libya kujitoa katika harakati za kuandaa
michauano hiyo kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe mnamo mwezi Agosti
mwaka 2014.
CAF walitangaza tena nafasi za kuomba uwenyeji wa
michuano hiyo na bingwa kutangazwa mwaka 2015 kwa ajili ya michuano kufanyika
mwaka 2017.
Nchi takribani saba zilijitosa katika kuwania nafasi
hiyo ikiwemo nchi ya Algeria, Misri, Gabon, Ghana, Kenya, Sudan, na Zimbabwe, huku
ni nchi nne peke ambazo zilikubaliwa na CAF ikiwemo Algeria, Misri, Gabon, na Ghana
kabla ya nchi ya Misri kujitoa kujitoa katika machakato huo.
Mnamo mwezi April mwaka 2015, rais wa CAF Issa Hayatou
alitangaza rasmi kuwa nchi ya Gabon itachukua nafasi ya kuandaa michuano ya
“AFCON” kwa mwaka 2017.
Cameroon
waweka rekodi nyingine kutwaa taji la Afcon.
Usiku wa Februari 5 ni usiku ambao kwa taifa la
Cameroon halitasahau katika mchezo wa soka baada ya kumuangusha farao wa Misri
kwa kutwaa taji la kombe la Mataifa ya Afrika “Afcon”.
Usiku huo ulikuwa mzito kuwa Misri kutokana na kutoka
katika fainali hizo za Mataifa ya Afrika maarufu kama AFCON 2017 wakiwa na
historia ya tofauti kwa kutolewa na nchi ya Cameroon.
Fainali ya AFCON 2017 ilikuwa unazikutanisha timu za
Misri dhidi ya Cameroon, lakini Cameroon wamefanikiwa kufuta uteja wa kufungwa
fainali mbili na Misri na kufanikiwa kutwaa taji hilo.
Cameroon sasa wanapata ushidi wa tano wa michuano hiyo
baada ya kufumgwa fainali mbili za AFCON na Misri,mnamo mwaka 2008 na 1986.
Yote kwa yote Cameroon sasa wameweka rekodi ya kuwa
timu ya kwanza kuwahi kuifunga Misri goli katika fainali za AFCON baada ya
Ethiopia, huku kocha wa Misri Hector Raul Cuper akiendeleza rekodi yake mbovu
kwa kupoteza fainali yake ya sita katika soka akiwa kama kocha wa timu tofauti.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.